Home Uncategorized NYOTA SPURS AWAFUATA MASHABIKI NA KUZOZANA NAO

NYOTA SPURS AWAFUATA MASHABIKI NA KUZOZANA NAO


NYOTA wa kikosi cha Tottenham Spurs, Eric Dier, usiku wa kumkia leo aliwafuata mashabiki na kuzozana nao baada ya timu yake kutolewa kwenye mchezo wa Kombe la FA, England na Norwich kwa penalti 3-2.

Licha ya Spurs kuanza kushinda dakika ya 13 kupitia kwa Jan Vertonghen bao hilo lilisawazishwa na Josip Drmic dakika ya 78 liliwapeleka kwenye hatua ya changamoto ya penalti ambapo Spurs ilifunga 2-3 za Norwich City.

Nyota huyo alifanya hivyo baada ya kuhisi kwamba Kaka yake alikuwa anabezwa na mashabiki kwa kitendo cha timu hiyo kushindwa kutinga robo fainali ya Kombe la FA England.

Kwa kitendo hicho nyota huyo adhabu inamuhusu. Kocha Mkuu wa Spurs, Jose Mourinho amesema kuwa familia ya Eric ilikuwa ndani ya uwanja na Kaka yake alifanyiwa kitu kisichopendaza lakini Eric naye amefanya jambo ambalo mchezaji hapaswi kufanya ila imetokea.

SOMA NA HII  MTUPIAJI NAMBA MOJA MBAO FC AMLILIA MKAPA, ATAJA SABABU ZA KUMKUMBUKA