Home Uncategorized WAWILI, BABA NA MWANA NDANI YA AC MILAN WAGUNDULIKA NA CORONA

WAWILI, BABA NA MWANA NDANI YA AC MILAN WAGUNDULIKA NA CORONA


KIONGOZI wa benchi la ufundi la AC Milan ya Italia, Paolo Maldini mwenye umri wa miaka 51 na mwanaye Daniel anayekipiga timu ya vijana ndani ya AC Milan mwenye umri miaka 18 wamekutwa na Virusi vya Corona.
Kwa mujibu wa chama cha soka cha Italia wawili hao wataendelea kukaa kwenye uangalizi maalumu kwa muda wa siku 14 ili kuuia maambukizi kwa wengine.
Uongozi wa Milan umesema kuwa  Paolo na Daniel Maldini wote kwa sasa wanaendelea vizuri kutokana na huduma ambayo wanapata kwa sasa.
Ujumbe wa AC Milan umesema kuwa: “AC Milan inathibitisha kwamba Paolo Maldini kiongozi kwenye benchi la ufundi amekutwa na Virusi vya Corona na alianza kuonyesha dalili kabla ya kugundulika ameathirika.
“Pia mwanaye ambaye ni mshambuliaji wa timu ya AC Milan ya vijana naye pia amegundulika na Virusi vya Corona.
SOMA NA HII  NAMUNGO WAREJEA BONGO