Home Uncategorized YANGA KWENYE KIBARUA KINGINE KESHO TAIFA

YANGA KWENYE KIBARUA KINGINE KESHO TAIFA

YANGA kesho inatarajiwa kushuka Uwanja wa Taifa kumenyana na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukukumbu ya kulazimishwa sare kwenye mchezo wao uliopita mbele ya KMC kwa kufungana bao 1-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na watapambana kupata matokeo.

“Wachezaji wapo tayari na kila mmoja anatambua majukumu yake nina imani kila kitu kitakuwa sawa ni suala la kusubiri na kuona itakuaje,” amesema.

Yanga imecheza mechi 25 kwenye ligi na imejikusanyia pointi 50 huku ikiwa na pointi 50 kibindoni.

SOMA NA HII  BREAKING:MANCHESTER CITY YASHINDA RUFAA YAKE YA KUSHIRIKI LIGI YA MABINGWA ULAYA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here