Home Uncategorized YANGA YATAJA ILIVYOWABANA SIMBA TAIFA, MASHABIKI WAPEWA TANO

YANGA YATAJA ILIVYOWABANA SIMBA TAIFA, MASHABIKI WAPEWA TANO


NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa ilikuwa ni mpango kazi wa wachezaji kucheza kwa kujituma mwanzo mwisho kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa watani wa jadi dhidi ya Simba na kuwashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi.

Simba ilikubali kuchapwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Machi 8 na kuziacha pointi tatu kusepa jumlajumla.

Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa wachezaji walipewa majukumu na kila mmoja alitimiza kile ambacho aliambiwa akifanye kwa wakati ndani ya uwanja.

“Wachezaji tulijituma uwanjani na tulikubaliana kufanya kazi kwa kushirikiana jambo ambalo lilitupa kujiamini na kufanya vizuri kwenye mchezo wetu ambao ulikuwa ni mgumu, shukrani kwa mashabiki kujitokeza wa wingi,” amesema. 

SOMA NA HII  YANGA KUMENOGA, MAMIMLIONI KAMA YOTE SASA MEZANI