Home Uncategorized YANGA:CORONA IMELETA WASIWASI

YANGA:CORONA IMELETA WASIWASI

JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo vinaleta wasiwasi ndani ya ardhi ya Bongo ni kusambaa kwa virusi vya Corona.
Abdul ambaye alikuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania iliyovunjwa kutokana na kusambaa kwa Virusi vya Corona amesema kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni maombi.
“Hili ni suala la dunia nzima na linaleta wasiwasi, kikubwa kinachotakiwa kwa sasa ni maombi na kufuata kanuni za afya kwani hakuna namna nyingine ya kufanya.
“Kwa sasa ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuondoa wasiwasi ambao upo, nina amini kwamba hili nalo litapita,” amesema Abdul.
SOMA NA HII  KOCHA YANGA:HARUNA NIYONZIMA HANA NIDHAMU