Home Uncategorized BRUNO TARIMO AJIPA UBALOZI NCHINI SERBIA

BRUNO TARIMO AJIPA UBALOZI NCHINI SERBIA

BRUNO Tarimo ‘Vifuaviwili’ bondia wa ngumi za kulipwa ambaye ni  bingwa wa International Super Feather Weight alioupata nchini Serbia kwa pointi mbele ya bondia Scheka Gurdijeljac raia wa Serbia amesema kuwa ameamua kuwa balozi wa kupambana na Virusi vya Corona.
Kwa sasa Vifuaviwili anaishi nchini Serbia ambapo anaendelea kufanya mazoezi ndani ya nyumba baada ya Serikali kuzuia watu kutoka nje ili kujikinga na Virusi vya Corona.
Akizungumza na Kijiwe cha Ndondi, Vifuaviwili alisema:”Ninaendelea na mazoezi nchini Serbia kwani hali bado haijawa shwari ila nimejipa ubalozi wa kupitia mitandao ya kijamii nikiwasisitiza watu wachukue tahadhari na wakae nyumbani,” alisema Vifuaviwili.
SOMA NA HII  BEKI WA MANCHESTER UNITED ASHINIKIZA KUSEPA MAZIMA