Home Uncategorized DIAMOND AMEANZA, WENGINE PIA NI WAKATI WA KUUNGANA NAYE, VITA NI YETU...

DIAMOND AMEANZA, WENGINE PIA NI WAKATI WA KUUNGANA NAYE, VITA NI YETU SOTE


WAKATI ule nakumbuka sio muda mrefu ngoma ya Kamwambie ilikuwa ni ya taifa ambapo kila kona ilikuwa inapigwa na watu wakawa wanaielewa.
Sikupata tabu sana kuelewa sababu ya watu kutambua vema ujumbe ule ilikuwa umegusa panapo kwa wale ambao walikuwa wanawatuma washkaji zao na jamaa ilikuwa ni sehemu ya kutokea.
Ila mwisho wa siku Kamwambie imebadilisha maisha ya wengi wapo ambao leo hii wapo pamoja ama wengine wanaendelea na mishe zao kama kawa ila ujumbe uliwafikia.
Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ndiye mtunzi wa ngoma hiyo ambayo bado haijafa inaishi mpaka sasa ila kutokana na muda mwingi kumeguka wengi wameipa kisogo.
Leo pia naja kwako mtunzi Diamond kama ambavyo ulikuwa ukimtuma rafiki yako akamwambie namI leo acha tu nikamwambie kwamba yale unayoyafanya yanapenya kwenye ngoma za maskio ya ulimwengu mzima.
Hivi karibuni Aprili, 25 ulitoa tamko kupitia kwenye ukurasa wako rasmi wa Istagram kwamba umeguswa na janga la Virusi vya Corona ambalo kwa sasa linaitikisa dunia.
Katika hilo ukafunguka kwamba unatambua wengi kwa sasa kwa watanzania ambao kipato chao na maisha yao ni Mungu mwenyewe anawapigania usiku na mchana ukaamua kujitoa kulipa kodi kwa kaya 500.
Hauna lengo baya pia umeeleza kwamba unahitaji kupunguza ukali wa maisha kwa kaya ambazo kipato chao ni cha chini, katika hilo unastahili pongezi.
Sasa jambo lenyewe ambalo ninahitaji kukwambia ni kwamba isiwe ni kujilisha upepo kwa wakati huu ukawaaminisha watu mia tano kwamba unatoa kodi ya pango kisha yakaanza mambo yako ya zile nyimbo zako.
Mara nataka kulewa sijui mawazo, ndugu yangu kama itakuwa ni katika hilo huko ni kujilisha upepo haina maana kuweka hadharani kisha mambo yakawa ndivyo sivyo.
Natambua Diamond unatambua kwamba mtaani mambo ni meusi kwa sasa hivyo ahadi ambayo umeahidi umegusa mioyo ya dunia nzima.
Wengi kwa sasa wanakuombea dua njema ili usiwe na mawazo ya kupindua meza kibabe bali utimize ahadi yako ambayo umeiahidi na Mungu atakujazi.
Lakini kama itatokea itakuwa kesho basi ndugu yangu yale maumivu ya zile dua za wale ambao walikuwa na matumaini zitakapoyeyuka itakuwa ni pigo kwako.
Ni wakati wa mwingine pia kwa wengine kuungana na Diamond katika hili kwani janga lipo na ni lazima tupambane na tusisahau kuchua tahadhari.
Afya ni moja ya utajiri ambao tumepewa na Mungu hivyo ikiwa utafanya makusudi mwenyewe kuupoteza itakuwa ngumu kufikia yale malengo uliyojiwekea.
Tuendelee kuchukua tahadhari huku tukiamini kwamba mambo yatakuwa sawa bila kusahau kufanya dua katika kila hatua.
Kwa Yule ambaye atapuuzia kufuata ule utaratibu uliowekwa na Serikali pamoja na Wizara ya afya basi ndugu yangu usisahau kumwambia.
SOMA NA HII  DILUNGA AWAOMBA RADHI MABOSI WAKE WA ZAMANI MTIBWA BAADA YA KUWATUNGUA