Home Uncategorized KIUNGO HUYU ANAYEKIPIGA KENYA AKUBALI KUSAINI YANGA

KIUNGO HUYU ANAYEKIPIGA KENYA AKUBALI KUSAINI YANGA

NEEMA imewaangukia Yanga baada ya meneja wa kiungo, Yidah Sven anayekipiga katika Klabu ya Kariobang Sharks ya Kenya, kukubali kumuachia mchezaji huyo kama Yanga itawasilisha ofa mezani ya kumsajili.
Yanga imekuwa moja ya klabu zinazohusishwa na usajili wa nyota huyo ambaye walivutiwa naye walipokutana na Kariobangs Sharks katika mchezo wa Siku ya Wananchi uliofanyika katika Uwanja wa Taifa na kumalizika kwa bao 1-1.
Meneja wa mchezaji huyo, Ronny Rusigi Ayumba, amesema kuwa Kariobang Sharks ipo tayari kumuachia mchezaji huyo endapo Yanga watawasilisha ofa ya kumsajili.
“Yanga kama kweli wanamhitaji Yidah wanatakiwa kuwasilisha ofa kwa uongozi wa Kariobang kwani wao wapo tayari kumuachia mchezaji huyo endapo watakamilisha taratibu zote za usajili.
“Siku hizi wachezaji ni kama bidhaa tu hata umzuie vipi lakini mwisho wa siku hata wao Kariobang watahitaji kununua mchezaji, hivyo lazima wakawasilishe ofa sehemu husika na ndio ambavyo Yanga wanatakiwa wafanye ili kumpata Yidah,” amesema meneja huyo.
Kwa upande wa mchezaji, Yidah Sven amesema kuwa yeye yupo tayari kuitumikia Yanga kwa kuwa ni timu kubwa, kama wapo tayari kumsajili yupo tayari kujiunga na timu hiyo.
“Nipo tayari kujiunga na Yanga kama kweli wananihitaji, Yanga ni timu nzuri na kubwa hapa Afrika, hivyo kuichezea timu hiyo kwangu litakuwa jambo zuri sana,” amesema kiungo huyo.
Chanzo:Championi
SOMA NA HII  KWA YANGA HII MJIPANGE!