Home Uncategorized KMC WAPIGA MATIZI YAO BINAFSI, HIVI NDIVYO WANAVYOFUATILIWA

KMC WAPIGA MATIZI YAO BINAFSI, HIVI NDIVYO WANAVYOFUATILIWA


UONGOZI wa KMC umesema kuwa kwa sasa wachezaji wote wamepewa program ya kufanya wakiwa kwenye mapumziko kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa wamekuwa wakiwafuatilia wachezaji wao kupitia mitandao ili kujua namna gani wanaendelea na mazoezi.

“Wachezaji wapo nyumbani kwa sasa wakiendelea na mazoezi binafsi ambayo wamepewa na benchi la ufundi.

“Ni ngumu kujua kwamba kwa namna gani wanaendelea ila tunashukuru Mungu kwa kuwa tunawaona kupita makundi yetu na hii inatupa nguvu ya kuamini kwamba wanafanya kile wanachoelekezwa pia tumewaambia wachukue tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona,” amesema.

SOMA NA HII  KMC KUANZA NA MAJEMBE 11 MAPYA HAYA HAPA