Home Uncategorized MESSI AJIFUNGIA NDANI KISA CORONA

MESSI AJIFUNGIA NDANI KISA CORONA


RAMADHAN Singano,’Messi’ nyota kutoka Bongo anayekipiga ndani ya TP Mazembe ya nchini Congo amesema kuwa kwa sasa anashinda ndani akifanya mazoezi mepesi kutokana na zuio la Serikali kutowaruhusu kutoka nje.
Virusi vya Corona vimekuwa ni janga la dunia baada ya kuripotiwa kuanza kusambaa ambapo  kesi ya kwanza iligundulika nchini China, Desemba 2019.
Messi amesema kuwa kutokana na janga la Corona kwa sasa wanaendelea kufanyia mazoezi nyumbani baada ya zuio la Serikali.
“Kwa sasa tupo tunaendelea salama ila kwa upande wa mazoezi tunapigia nyumbani kwani hakuna ruhusa ya kuwa nje kutokana na kujikinga na Virusi vya Corona, ni maombi yetu hali iwe salama turudi kwenye wakati wetu kama zamani,” amesema Messi.
SOMA NA HII  ASTON VILLA TAYARI KWA SAMATTA, YAKUBALI KUMWAGA KITITA CHA PAUNI MILIONI 10

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here