Home Uncategorized MLINDA MLANGO KAGERA SUGAR APATA MUDA WA KULEA BINTI WAKE

MLINDA MLANGO KAGERA SUGAR APATA MUDA WA KULEA BINTI WAKE


BENEDICT Tinoko, mlinda mlango wa Kagera Sugar amesema kuwa likizo ya lazima waliyopewa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona imempa nafasi ya kumwona binti yake.

Binti huyo aliletwa duniani wakati kipa huyo akitimiza majukumu yake ndani ya Klabu ya Kagera Sugar.

Nyota huyo amesema:-“Ukweli ni kwamba Corona imeharibu kwa kiasi kikubwa shughuli zetu lakini kwa upande wangu namshukuru Mungu kwani licha ya changamoto zote hizo nimepata nafasi ya kukutana na binti yangu.


 “Kutokana na hali hiyo sikuwa na nafasi ya kumwona wakati ligi inaendelea sasa nafurahia kumlea mtoto wangu pamoja na kuendelea na ratiba za mazoezi,”.

 Kagera Sugar ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 41 baada ya kucheza mechi 29.

SOMA NA HII  DEO KANDA ATAJWA KUIBUKIA YANGA