Home Uncategorized MTUPIAJI MWINGINE HUYU WA CONGO AINGIA ANGA ZA YANGA

MTUPIAJI MWINGINE HUYU WA CONGO AINGIA ANGA ZA YANGA

LELO Amfumu ni nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Rangers inayoshiriki Ligi Kuu nchini Congo.

Nafasi yake ni ushambuliaji na ni miongoni mwa washambuliaji ambao wanafanya vizuri kwenye ligi hiyo yenye timu kubwa Afrika ikiwa ni pamoja na AS Vita pamoja na TP Mazembe.

Kwenye washambuliaji wenye mabao zaidi ya saba naye yumo akiwa ametupia mabao tisa na anashika nafasi ya tano kwa wafungaji ndani ya ligi yao huku kinara wao akiwa ni Fiston Mayele wa AS Vita Club mwenye mabao 12.

Inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za mabosi wa Yanga ili akaongeze nguvu ndani ya kikosi msimu ujao.

SOMA NA HII  MTAMBO MPYA WA MABAO YANGA WAAHIDI UBINGWA