Home Uncategorized SIMBA YAKUBALI UWEZO WA KIUNGO WA YANGA ALIYEWAVURUGA MACHI 8 UWANJA WA...

SIMBA YAKUBALI UWEZO WA KIUNGO WA YANGA ALIYEWAVURUGA MACHI 8 UWANJA WA TAIFA

Verified

OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa miongni mwa viungo makini wanafaya kazi kwa ubora ndani ya Uwanja ni pamoja na Feisal Salum ’Toto’ anayekipiga ndani ya Yanga.

Fei Toto atakumbukwa msimu huu walipokutana Machi 8 Uwanja wa Taifa kwa kuwavuruga viugo wa Siba chini ya mwamba wa Lusaka, Clatous Chama.

Mchezo huo Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 lililolpachikwa kimiani na Bernard Morrison.

Manara amesema:”Moja ya kiungo aliyejaaliwa uwezo mkubwa uwanjani, alitabiriwa na Kocha Emmanuel Amunike kufanya makubwa zaidi. Bado hajatupa alichonacho kwa asilimia 100%, labda anahitajika kujua nn kesho yake ijayo,” .

SOMA NA HII  AZAM FC YAHAMIA SASA KWENYE JUKWAA