UONGOZI wa Simba umesema kuwa Yanga walistahili kushinda mechi yao iliyochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa kutokana na kuwazidi mbinu.
Yanga iliwashinda Simba kwa kuifunga bao 1-0 bao lililofungwa na Bernard Morrison dakika ya 44.
Habari kutoka ndani ya Uongozi wa Simba zimeeleza kuwa walistahili kuchapwa kwenye mechi hiyo kwa kushindwa kufanya vizuri.
“Tulistahili kufungwa kwa kuwa hatukufanya vizuri na wapinzani wetu walipiga mpira mwingi na pasi za maana kuliko sisi, haikuwa kazi rahisi licha ya wachezaji kujituma.
“Wachezaji wao walikuwa wanagongana na walicheza kwa kujituma jambo ambalo liliwabeba ila hatukuwa na namna tuliamini tungerudisha bao ila haikuwa hivyo,” alieleza kiongozi huyo.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa alishindwa kuendelea kuutazama mpira baada ya kufungwa jambo lililomkosesha raha.
“Sikuwa Bongo nilitazama mpira nikiwa nje ya Bongo tulipofungwa hali haikuwa shwari kwangu,” alisema.
Home Uncategorized UONGOZI WA SIMBA: TULISTAHILI KUFUNGWA NA YANGA, BOSI MMOJA ALISHINDWA KUMALIZA KUUTAZAMA...