Home Uncategorized VITALIS MAYANGA HAELEWI KILICHOMFANYA AWE BUTU NDANI YA KMC

VITALIS MAYANGA HAELEWI KILICHOMFANYA AWE BUTU NDANI YA KMC


VITALIS Mayanga mshambuliaji anayekipiga ndani ya Ndanda FC amesema kuwa mpaka sasa haelewi kilichomkwakmisha kufunga mabao alipokuwa ndani ya Klabu ya KMC.

Mayanga alipewa dili la miaka miwili ndani ya KMC mkataba wake ulivunjwa baada ya mabosi kushindwa kuelewa uwezo wake na alisepa akiwa hajafunga bao hata moja.

Mayanga ambaye alipoibuka ndani ya Ndanda amekuwa akicheka na nyavu kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Coona na alipewa tuzo ya mchezaji bora mwezi Machi.

Dili lake ndani ya Ndanda FC  ni la muda wa miezi mitano baada ya mabosi zake KMC kumpa barua ya kusepa mazima ndani ya klabu hiyo.
“Hata sisi wachezaji tulikuwa tunashangaa kwani katika timu za Ligi Kuu Bara ambazo zilikuwa zinafanya mazoezi ya nguvu ambayo hata sijawahi kufanya kwenye timu nyingine, ni pamoja na KMC, kwani tulikuwa tunacheza vizuri lakini kukawa na tatizo la kutofunga mabao, nafikiri tatizo lilikuwa hapo,” amesema.

 Kwa sasa ndani ya Ndanda FC ametupia mabao sita ambayo anayo kwa sasa.
SOMA NA HII  KMC YATUMA SALAMU KWA BIASHARA UNITED