Home Uncategorized YANGA WABISHI KWELI, WAIKOMALIA SIMBA KWA CHAMA

YANGA WABISHI KWELI, WAIKOMALIA SIMBA KWA CHAMA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umefikia hatua nzuri ya kuipata saini ya nyota wa Simba, Clatous Chama ili akacheze ndani ya Yanga msimu ujao.

Chama amekuwa gumzo kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja jambo ambalo limewavutia Yanga ambao wanahitaji kuboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wamezungumza na meneja wa Chama ambaye amesema kuwa mkataba wa nyota huo umebakisha miezi sita.

“Tupo kwenye mpango wa kumpata mchezaji wa Simba na tumezungumza na Meneja ambaye amesema kuwa mteja wake ana miezi sita hivyo ikiwa tunahitaji kumpata ni suala la muda tu,” amesema.

Chanzo: Wasafi

SOMA NA HII  BREAKING: NTIBANZOKIZA AMPOTEZA CHAMA BONGO, ASEPA NA TUZO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here