Home Uncategorized AGUERO MTUPIAJI NAMBA MOJA NDANI YA CITY NA HESABU ZA KUSEPA

AGUERO MTUPIAJI NAMBA MOJA NDANI YA CITY NA HESABU ZA KUSEPA


MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero anaweza kusepa ndani ya kikosi hicho pale mkataba wake utakapomeguka.

Mkataba wake unafika tamati mwaka 2021 na inaelezwa kuwa ana mpango wa kurejea Klabu yake iliyomkuza ya Independiente ya Argentina.


Nyota huyo raia wa Argentina mwenye miaka 31 alijiunga na City akitokea Klabu ya Atletico Madrid alikodumu kuanzia msimu wa 2006/11.


Mshambuliaji huyo ndani ya Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la Ligi Kuu England ametupia jumla ya mabao 254 na ndiye namba moja kwa kufunga mabao mengi ndani ya kosi hilo.

SOMA NA HII  KATI YA MORRISON, TUNOMBE,KISINDA,SARPONG, HUYU HAPA AMEWAPOTEZA WOTE