Home Uncategorized BALAA LA LAMINE MORO BEKI KISIKI WA YANGA LIPO NAMNA HII

BALAA LA LAMINE MORO BEKI KISIKI WA YANGA LIPO NAMNA HII


LAMINE Moro, beki wa kati wa Yanga msimu huu wa 2019/20 ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza ligi ya Bongo ameonyesha uimara na kuaminika na Kocha Mkuu, Luc Eymael.


Licha ya kwamba anamiliki bao moja ambalo alijifunga mbele ya Mbeya City Uwanja wa Taifa wakati Yanga ikiazimisha sare ya kufungana bao 1-1 amekuwa imara katika nafasi yake.

Ametumia dakika 1,433 uwanjani. Yanga ikiwa imecheza mechi 27 ameanza mechi 18 kwenye mechi za ligi.


Hizi hapa mechi zake:-Ruvu Shooting (90), Polisi Tanzania (90), JKT Tanzania (90), Alliance (90), KMC (90), Mbeya City (90), Prisons (90), Biashara United (90), Kagera Sugar (90), Azam FC (90), Singida United (90), Mtibwa Sugar (90), Lipuli (90), Ruvu Shooting (90), Mbeya City (90) Mbao (83), Simba (90), KMC (90).

Yanga imefungwa jumla ya mabao 20 ikiwa ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  TAMKO LA JPM JUU YA WALIOJENGA MABONDENI - VIDEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here