Home Uncategorized CORONA ILIVYOMTIBULIA TSHABALALA KULIPIZA KISASI SIMBA

CORONA ILIVYOMTIBULIA TSHABALALA KULIPIZA KISASI SIMBA


BEKI na Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema uwepo wa virusi vya corona umemtibulia mambo yake mengi ikiwemo kushindwa kulipiza kisasi kwa wachezaji wenzake.


Tshabalala ambaye ni beki tegemeo ndani ya kikosi hicho, amesema corona imemtibulia kilipa kisasi kwa wale wote ambao walimgaragaza wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.


Novemba 1, mwaka jana, Tshabalala ilikuwa siku yake ya kuzaliwa ambapo wachezaji wenzake wakiongozwa na beki mkongwe, Erasto Nyoni na kipa Aishi Manula, walimfanyia kitu mbaya kwa kumchafua vibaya na matope mara baada ya kumaliza mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana jijini Dar.


“Ujue hii corona imekuja kuharibu mambo mengi, hapa kati kuna birthday nyingi zimepita halafu hatujafanya chochote kwa wale wabaya wangu, aisee inaniuma sana.


“Hapa tukirudi tena kambini nitaanza na mmoja baada ya mwingine kwa wale wote ambao birthday zao ziliangukia kipindi ambacho hatupo kambini, lazima nilipize kisasi,” alisema Tshabalala.


Tangu kusimama kwa ligi Machi 17, mwaka huu kutokana na uwepo wa virusi vya corona, zimepita birthday kadhaa za wachezaji na viongozi wa Simba.


Birthday hizo ni; Jonas Mkude (Aprili 1), Ally Salim (Aprili 19), Rashid Juma (Aprili 21), Yusuf Mlipili (Aprili 22) na Kocha Msaidizi, Seleman Matola ( Aprili 24)
SOMA NA HII  LUKAKU WA MOTO KINOMA, CONTE KUJUA HATMA YAKE KESHO AKISHINDWA KUFURUKUTA MBELE YA SEVILLA