Home Uncategorized GANZI YA CORONA INAPOONGEZEWA NA ILE YA BILIONI MOJA YA MAGUFULI LAZIMA...

GANZI YA CORONA INAPOONGEZEWA NA ILE YA BILIONI MOJA YA MAGUFULI LAZIMA UVURUGIKE


ULIMWENGU wa michezo ukiwa unapiga hesabu namna gani hali itakuwa shwari kwa sasa ndani ya Bongo kwa ligi kurejea kuna ganzi nyingine imeibuka tena.

Ukiachana na janga la Virusi la Corona ambalo linaivurugavuruga dunia kwa sasa kuna habari nyingine tena imeanza kugonga kwenye vichwa vya familia ya michezo.
Jambo lenyewe ni sakata la bilioni moja iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuaandaa michuano ya Vijana iliyofanyika Bongo.
Michuano ya Cecafa ilituacha na ganzi moja matata ambayo bado inaishi mpaka sasa tena nyingine inaibuka ni kuhusu matumizi ya mkwanja huo.
Tumeona Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania,(Takukuru) imeeleza kuwa inafanya uchunguzi kuhusu matumizi ya mkwanja huo.
Hebu nikukumbushe kidogo mwaka 2019, Tanzania walikuwa wenyeji wa michuano ya Cecafa ya Vijana chini ya miaka 17.
Mwisho wa siku Tanzania iliambulia kupigwa kwenye mechi zake zote ilizocheza na ilimaliza mashindano ikiwa mikono mitupu bila hata pointi moja.
Sasa kuna bilioni moja ambayo Magufuli alisema ametoa kwa ajili ya mashindano ya vijana na ilikuwa mbele ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) Wallace Karia.
Baada ya Takukuru kueleza kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu matumizi ya mkwanja huo uliotolewa na Serikali ghafla kuna picha nyingine inatolewa pale TFF.
Taarifa inaeleza kuwa hakuna mkwanja ulioingia kwenye akaunti ya TFF kwa ajili ya michuano ya Cecafa sasa hapo ndipo ninashindwa kuelewa kipi ni kipi.
Jambo hili linafikirisha kweli na lazima kila mdau akae chini afikiri mara mbili kuna nini ambacho kipo nyuma ya mkwanja mrefu ambao ni bilioni moja?
Kama wenye mamlaka wenyewe ambao wanachunguzwa na hawatambui kwamba kuna mkwanja uliingizwa ulikwenda wapi?
Kuna mambo mengine wanafamilia ya michezo tukifiria sana tunapasua tu vichwa vyetu ngoja tusubiri na tuone picha hili litakwishwaje maana tayari picha limeshaanza.
Yote kwa yote bado tunakazi kubwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ambayo ipo na inaumiza wengi wameanza kupuuzia hili.
Tusiache kufanya yale ambayo tunaelekwezwa na wataalamu kwa kuwa afya ni muhimu na familia ya michezo inapenda kuona watu wakiwa katika afya zao muda wote.
Umakini unahitajika kila saa kila wakati ili kuona nana gani iwapo ligi itarejea tutashuhudia ile burudani ambayo tuliikosa kwa muda mrefu.
Picha la makao makuu pale Karume tutaendelea kulifuatilia kwa ukaribu ili kujua haya mambo yanakuajekuaje kwa sasa.
SOMA NA HII  DITRAM NCHIMBI: NINACHUKUA TAHADHARI YA CORONA NA KULINDA KIPAJI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here