Home Uncategorized JUMA MAHADHI AWAPA AHADI MASHABIKI WA YANGA

JUMA MAHADHI AWAPA AHADI MASHABIKI WA YANGA


JUMA Mahadhi, winga wa Yanga amesema kuwa kwa sasa yupo vema anatarajia kurejea uwanjani pale ligi itakaporejea.

Mahadhi alikuwa nje msimu mzima akiuguza jeraha la goti alilopata 2018/19 na tayari ameshaanza mazoezi ili kuimarisha uwezo wake.

“Nipo fiti kwa sasa ninatarajia kurejea uwanjani pale ligi itakapoanza hivyo mashabiki watarajie makubwa kutoka kwangu,” amesema.

Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kurejea hivi karibuni ambapo ilisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA KWA KUCHECHEMEA, COASTAL UNION YAZINDUKA