Home Uncategorized KAGERA SUGAR V YANGA MECHI YA KISASI

KAGERA SUGAR V YANGA MECHI YA KISASI


KLABU ya Kagere Sugar iliyo chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime imeshaanza maandalizi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Jana ilipopangwa ratiba ya hatua ya robo fainali, Kagera Sugar itakutana na Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael.

Kagera Sugar kwenye mechi ya kwanza walipokutana na Yanga kwenye ligi kuu iliwanyoosha kwa mabao 3-0.

Ikumbukwe kuwa mechi hiyo ilikuwa ni ya kwanza kwa Mbelgiji Eymael baada ya kukabidhiwa mikoba ya Mwinyi Zahera.

Kazi itakuwa kubwa Juni 27/28 Uwanja wa Taifa ambapo itakuwa ni mechi ya kisasi.

Tayari imeshaanza mazoezi huku ikiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

SOMA NA HII  MWENGE WAFIKIWA NA MERIDIAN BET