Home Uncategorized KIUNGO WA YANGA HUMWAMBII KITU KUHUSU UGALI

KIUNGO WA YANGA HUMWAMBII KITU KUHUSU UGALI

BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa miongoni mwa vyakula ambavyo anapenda kula ni ugali.
Morrison raia wa Ghana alitua Desemba akitokea nchini Ghana kwenye usajili wa dirisha dogo mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara akiwa amecheza mechi 10 amefunga mabao matatu huku akiwa na bao moja kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Kiungo huyo amesema:”Ninapenda kula ugali kwani ni chakula ambacho huwa ninafurahia ninapokula kwa kuwa kinanipa nguvu na kunifanya nijiskie vizuri.
“Kwa sasa ninaendelea na mazoezi binafsi ili kulinda kipaji changu ili ligi ikirejea niwe kwenye ubora ambao nilikuwa nao,” amesema.
Timu ambazo amezitungua Morrison ni pamoja na Tanzania Prisons mchezo wa Kombe la Shirikisho huku Lipuli, Mbeya City na Simba akizitungua kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.
SOMA NA HII  ARUSHA FC YAIPIGIA HESABU KALI GIPCO