Home Uncategorized LIGI KUU BARA IKIBONYEZEWA CHEKUNDU, REKODI HIZI ZINAKWENDA NA MAJI

LIGI KUU BARA IKIBONYEZEWA CHEKUNDU, REKODI HIZI ZINAKWENDA NA MAJI


KWA sasa ni dua ambazo zinaendelea kuombwa ili ule uhondo wa Ligi Kuu Bara uweze kurejea upya na burudani iendelee pale ilipoishia.
Kumekuwa na mabadiliko ya mambo mengi kwa sasa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambayo vimesimamisha mambo mengi huku hata ishu kurejea kwa ligi ikiwa bado haijajulikana.
Iwapo ikitokea ligi ikafutwa kuna mambo mengi ambayo yatawaumiza wengi na kufanya rekodi zao walizoweka kuyeyuka jumlajumla.
Baadhi ya mambo ambayo yatakaa vichwani mwa mashabiki na wachezaji iwapo ligi itafutwa licha ya kwamba hakuna anayependa iwe hivyo kwa sasa haya hapa :-
Bao la Morrison
Machi 8, Uwanja wa Taifa mashabiki wa Yanga wakiwa nyumbani kwenye mchezo wa mzunguko wa pili walitoka uwanjani wakiwa vifua mbele kwa ushindi walioupata mbele ya Simba.
Ushindi huo waliupata kwa bao pekee lililofungwa nje ya 18 na kiungo, Bernard Morrison dakika ya 44 kwa mpira wa adhabu ambao ulizima mazima kwenye nyavu.
Iwapo ikatokea ligi ikafutwa wanajangwani hawatakuwa na furaha kwa kuwa rekodi ya kushindwa kuifunga Simba kwa muda wa misimu mitatu mfululizo itabaki palepale.
Tangu msimu wa 2016/17 Yanga ilikuwa haijaitungua Simba ilikuja kuwatungua Simba baada ya misimu mitatu kumeguka hivyo msimu ukifutwa rekodi hilo bao litabaki kichwani.
Wakali wa hat-trick
Haikuwa bahati kwa Singida United msimu huu ilikuwa inapokea vichapo na kuacha mipira ikisepa. Huenda msimu ukifutwa kwao wataachia tabasamu la moyoni ila maamuzi hayo yatawaumiza wale waliopiga hat trick.
Wachezaji sita walisepa na mipira ambapo mfunguzi wao alikuwa ni Ditram Nchimbi aliwatungua Yanga wakati huo alikuwa Polisi Tanzania, Daruesh Saliboko wa Lipuli  aliwatungua Singida United, Obrey Chirwa wa Azam FC mbele ya Alliance, David Richard wa Alliance ilikuwa kwa Mwadui FC, Kelvin Sabato wa Kagera Sugar aliwatungua Singida United na Meddie Kagere aliiadhibu Singida United.
Wazawa na nyavu
Ishu ya kiatu cha ufungaji bora ilikuwa na ushindani mkubwa kwani licha ya mnyarwanda Meddie Kagere kutupia mabao 19 bado wazawa walikuwa wanakuja. Huenda tungeshuhudia mapinduzi kwa wazawa kusepa na kiatu cha ufungaji bora.
Relliats Lusajo wa Namungo FC, Paul Nonga wa Lipuli na Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar hawa walikuwa wamewasha taa nyekundu ambapo kila mmoja alikuwa ametupia mabao 11 hivyo msimu iwapo utafutwa mabao yao pia yatayeyuka mazima na kubaki vichwani mwao.
Wakali wa asisti
Kwa msimu uliopita baba lao alikuwa ni Ibrahim Ajibu alipokuwa Yanga ambapo rekodi yake bado haijavunjwa alipotoa asisti 17 na mabao sita.
Kwa msimu huu vita kubwa ni kati ya Nicolaus Wadada wa Azam FC na Clatous Chama wa Simba ambao wote wametoa asisti saba iwapo msimu huu utabonyezewa chekundu hawatakuwa na rekodi hizi tamu ambazo wameziweka itauma kinoma.
Wazee wa mipira iliyokufa
Mzawa anayekipiga Mbeya City, Peter Mapunda ndiye baba lao kwani amefunga mabao sita kwa penalti kati ya mabao tisa aliyonayo. Mkali mwingine ni Meddie Kagere yeye ametupia mabao matatu kwa penalti kati ya mabao 19 sawa na David Molinga wa Yanga ambaye yeye mabao mawili alifunga kwa faulo za moja kwa moja na bao moja kwa penalti kati ya yale nane aliyonayo.Ikibonyezewa chekundu rekodi hizi zitaishi vichwani ila kwenye kumbukumbu hazitakuwepo.
Wakali wa kuokoa penalti
Makipa nao wamo iwapo msimu utabonyezewa chekundu itawauma, rekodi zao walizoweka wakiwa langoni.Razack Abarola wa Azam FC aliokoa mchomo wa Sixtus Sabilo wa Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru. Daniel Mgore wa Biashara United aliokoa penalti ya Meddie Kagere wa Simba Uwanja wa Taifa. Iwapo msimu utafutwa mambo yataanza upya.
Wapindua meza kibabe
Ndanda FC Februari 29 ilipindua meza kibabe mbele ya Lipuli ambayo ilikuwa inaongoza kwa mabao matatu na mwisho wa dakika 90 ngoma ikaisha kwa sare ya kufungana mabao 3-3. Januari 4 itawaumiza watani wa Simba ambao ni Yanga iwapo itafutwa kwani Simba ilianza kuifunga Yanga mabao 2 ila mwisho wa dakika 90 ngoma ilikuwa ni 2-2.
SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA LEO DHIDI YA KAGERA SUGAR