Home Uncategorized MABOSI AZAM FC WATEMBEZA MKWARA MZITO KWA SIMBA

MABOSI AZAM FC WATEMBEZA MKWARA MZITO KWA SIMBA


UONGOZI wa Azam FC umeionya Simba juu ya beki wao Yakub Mohamed ambaye anahusishwa kujiunga na mabingwa hao watetezi kwa kusema kuwa hawaruhusiwi kufanya naye mazungumzo kwa kuwa bado ana mkataba na Azam FC.

Imekuwa ikiripotiwa kuwa Simba ipo kwenye hesabu za kuipata saini ya beki huyo ili akaungane na Pascal Wawa, Erasto Nyoni kusongesha gurudumu ndani ya Simba.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdululkarim Amin, amesema kuwa ni kosa la kisheria kwa klabu yoyote kufanya mazungumzo na mchezaji wao Yakub kwani bado ana mkataba.

“Yakub ni mali ya Azam FC bado ana mkataba kwa sasa hivyo ni kosa kisheria kufanya naye mazungumzo ikibainika kwa klabu yoyote ile tutaichukulia hatua kwa kuwa ni makosa,” amesema.

Tayari Azam FC imemuongezea kandarasi ya mwaka mmoja mshambuliaji wao namba moja Obrey Chirwa ambaye alikuwa anahusishwa kujiunga na Yanga.

SOMA NA HII  NEYMAR AAMBULIA KADI NYEKUNDU TIMU YAKE IKICHAPWA BAO 1-0