Home Uncategorized NYOTA HAWA TISA NDANI YA SIMBA MSIMU UKIMEGUKA TU WANAWEZA KUSEPA BURE...

NYOTA HAWA TISA NDANI YA SIMBA MSIMU UKIMEGUKA TU WANAWEZA KUSEPA BURE KABISA


SIMBA ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zake 71 kibindoni kuna mastaa ambao maisha yao yanafika ukingoni mwishoni mwa msimu ligi ikikamilika.

Ikiwa hawatamalizana na mabosi wao Simba kwa sasa basi itakuwa njia nyeupe kwao kusepa timu nyingine bure kabisa.

Mastaa hao ni pamoja na kiungo machachari ndani ya uwanja Shiza Kichuya maarufu kama Kichuya kona, Hassani Dilunga, beki kisiki Pascal Serge Wawa raia wa Ivory Coast.

 Yusuph Mlipili beki mzawa wa kati ambaye maisha yake msimu huu yamekuwa ya tabu kikosi cha kwanza, Sharaff Eldin Shiboub kiungo raia wa Sudan.

Marcel Kaheza anayekipiga Polisi Tanzania kwa mkopo, Mohamed Rashid yeye yupo zake JKT Tanzania, Mohamed Ibrahim,’Mo Ibra’ anayekipiga Namungo pamoja na Paul Bukaba ambaye yupo zake ndani ya Namungo.

SOMA NA HII  GREALISH: MASHINE ASTON VILLA ITAKAYOJUMLISHA NGUVU NA SAMATTA, KUSAKA UKOMBOZI