Home Uncategorized TIMU ZINAZOTAKA SAINI YA MWAMNYETO INABIDI ZIVUNJE TU BENKI HAMNA NAMNA

TIMU ZINAZOTAKA SAINI YA MWAMNYETO INABIDI ZIVUNJE TU BENKI HAMNA NAMNA

INAELEZWA kuwa thamani ya beki wa Coastal Union,  Bakari Mwamnyeto inafika milioni 85 hivyo timu inayomtaka ivunje benki kuweka mkwanja huo mezani.

Beki huyo chipukizi anavaa kitambaa cha unahodha ndani ya klabu hiyo iliyo chini ya Kocha Mku

u, Juma Mgunda.

Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuiwinda saini yake ni pamoja na Simba iliyo chini ya Sven Vandenbroec pamoja na Yanga iliyo chini ya Luc Eymael wote ni raia wa Ubelgiji.

Pia matajiri wa Bongo, Azam FC wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kuwania saini yake ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho ambao ni Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho.

Mwamnyeto amesema:”Nimekuwa nikiskia taarifa hizo ila hakuna kitu kinachoendelea nipo zangu bado ndani ya Coastal Union,”.

SOMA NA HII  HAJI MANARA WA SIMBA ALA DILI AZAM MEDIA