Home Uncategorized YIKPE MSHAMBULIAJI WA YANGA AOMBA APEWE MUDA KUONYESHA MAAJABU

YIKPE MSHAMBULIAJI WA YANGA AOMBA APEWE MUDA KUONYESHA MAAJABU

YKIPE Gislain amesema kuwa anaomba apewe

muda zaidi ndani ya Klabu ya Yanga ili kuonyesha ujuzi wake wote.

Nyota huyo alisajiliwa akitokea Klabu ya Gor Mahia ambapo alivunja mkataba wake ili kukipiga ndani ya Klabu hiyo Desemba mwaka jana.

Ameshindwa kufurukuta ndani ya Yanga ambapo amefunga bao moja ndani ya Ligi Kuu Bara ilikuwa mbele ya Singida United wakati Yanga ikishinda mabao 3-1.

Yikpe amesema:” Nataka kuondoka ndani ya Yanga nikiwa nimeweka historia na kufanya makubwa kwa ajili ya timu yangu hivyo ninahitaji nafasi. “Nimeshindwa kufanya makubwa kwa kuwa nilikuwa sipati nafasi nikipata nafasi pale ligi itakaporejea sitafanya makosa,”.

SOMA NA HII  PACHA WA MWAMNYETO, AME, PICHA ZIMA KUIBUKIA SIMBA LIMECHEZWA HIVI