Home Uncategorized FILAMU YA BERNARD MORRISON NI PASUA KICHWA NDANI YA YANGA, GSM WAFUNGUKA...

FILAMU YA BERNARD MORRISON NI PASUA KICHWA NDANI YA YANGA, GSM WAFUNGUKA ISHU YA MKATABA WAKE


INJINIA Hersi Said amesema kuwa mchezaji wa Yanga, Bernard Morrison amesaini kandarasi ya miaka miwili mbele ya macho yake hivyo ni mali halali ya Yanga kwa sasa.

Injinia Said ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao wanashiriki katika masuala ya usajili wa Yanga amesema kuwa hakuna mjadala kuhusu mkataba wa Morrison kwa kuwa ameshasaini kandarasi ya miaka miwili kinachotokea kwa sasa amepewa mkataba na timu nyingine.

Said ameongeza kuwa alifuatwa na Morrison akiomba kuvunja mkataba ili asajiliwe kwenye timu ambazo zimehitaji kupata saini yake ili asaini kwenye timu hizo.

“Morrison alinifuata aliniambia kwamba anaomba avunje mkataba wa miaka miwili ambayo alikuwa amesaini kwa kuwa amepata klabu ambayo inampango wa kumpa dili na itamlipa vizuri zaidi.

“Nilichomwambia mimi ni kwamba kama anahitaji kuvunja mkataba ni lazima utaratibu ufuatwe kwani yeye kwa sasa ni mali ya Yanga hivyo ni lazima klabu ambazo zinahitaji saini yake zizungumze na uongozi wa Yanga.

“Kinachomsumbua kwa sasa ni tamaa anahitaji kupata fedha nyingi baada ya kuona kwamba kuna timu nyingi zinamhitaji ila ukweli ni kwamba yeye ni mchezaji wa Yanga na mazungumzo ya yeye kuondoka ni lazima yafanyikwe kwenye timu,” amesema. 

Leo gazeti la Championi Jumatano ambalo lipo mtaani limeandika kuwa Morrison ana mkataba wa miezi sita na ni mchezaji mwenyewe amesema.

Kuna mambo mengi amezungumza hali iliyopelekea apigwe faini na uongozi wa Yanga pia

SOMA NA HII  BIASHARA UNITED KAMILI KUMALIZANA NA SIMBA