Home Uncategorized GWAMBINA FC WAIVUTIA KASI TRANSIT CAMP, KESHO

GWAMBINA FC WAIVUTIA KASI TRANSIT CAMP, KESHO


GWAMBINA FC vinara wa kundi B kwenye Lgi Daraja la Kwanza wameendelea na mazoezi yao kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Transti Camp utakaochezwa kesho Uwanja wa Uhuru.

Ikiwa na pointi zake 40 nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 18 inahitaji pointi tatu ili kukamilisha safari yake ya kuanza kushiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.

Wanaowafuata Gwambina ni Geita Gold wakiwa na pointi 30 nao pia wamecheza mechi 18 ndani ya kundi B.

Transit Camp wapinzani wa Gwambina FC ipo nafasi  ya tano na kibindoni ina pointi 25 baada ya kucheza mechi 18.

Iwapo Gwambina itashinda kesho itajihakikishisha nafasi ya kushiriki Ligi Kuu Bara ikiwa na mechi mkononi.

SOMA NA HII  SHEVA, KIUNGO MZAWA HIVI NDIVYO ALIVYOZUIA USAJILI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here