Home Uncategorized JADON SANCHO NA AKANJI WAPIGWA FAINI KISA KUTOVAA BARAKOA

JADON SANCHO NA AKANJI WAPIGWA FAINI KISA KUTOVAA BARAKOA


JADON Sancho na mchezaji mwenzake Manuel Akanji wanaokipiga ndani ya Klabu ya Borussia Dortumund inayoshiriki Bundesliga wamepewa adhabu na chama cha Soka la Ujerumani (DFL) kwa kosa la kuonekana wakinyolewa bila kuvaa barakoa.
Kwa sasa dunia inapambana na janga la Virusi vya Corona ambalo linaivurugavuruga dunia jambo ambalo lilifanya chama cha soka cha Ujerumani kutoa taratibu ambazo zinapaswa zifuatwe mara moja kwa wachezaji.
Sancho alisambaza picha akiwa ananyolewa akiwa hajavaa barakoa sawa na mwenzake Akanji ambaye naye hakuvaa barakoa wakati akiwa saloni jambo lililofanya wapewe adhabu.
Akanji amepigwa faini ya dola 8,000 huku Sancho akitozwa faini ya dola 10,000 ili iwe fundisho kwa wengine wasifanye makosa hayo.
Baada ya adhabu hiyo Sancho alitweet kwa maneno mafupi kwenye akaunti yake ya twiter ambapo aliandika huu ni utani zaidi DFL.

Wachezaji hao wamepewa siku tano za kukata rufaa iwapo watakuwa na utetezi wa kwa nini walifanya jambo hilo,
SOMA NA HII  ARSENAL YAMTAKA KIUNGO WA SEVILLA