Home Uncategorized JONAS MKUDE NA BERNARD MORRISON WAKUTANA NA PANGA LA TFF

JONAS MKUDE NA BERNARD MORRISON WAKUTANA NA PANGA LA TFF


KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imewafungia wachezaji  Bernard Morrison kiungo wa Yanga na Jonas Mkude wa Simba michezo miwili kwa kila mmoja.

Mbali na adhabu hiyo  pia wamepigwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kutokana na vitendo ambavyo si vya kiungwana. Adhabu hiyo inaanza leo.

Leo Yanga inashuka uwanjani kumenyana na Namungo FC, Uwanja wa Taifa mechi itakayoanza saa 1:00 usiku.

Morrison amekumbana na adhabu hiyo baada ya kumpiga kwa kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.


Mchezo huo Yanga ililazimisha sare ya bila kufungana ulikuwa ni wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

 Jonas Mkude kiungo mkabaji wa Simba yeye alifanya hivyo kwa mchezaji wa Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 3-1 Uwanja wa Taifa.

Leo Simba itamenyana na Mbeya City Uwanja wa Sokoine, majira ya saa 10:00 jioni.

SOMA NA HII  MASAU BWIRE AJA NA KUPAPASA NA KUKUNG'UTA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here