Home Uncategorized KAGERE AFUNGUKIA MATESO YA MABAO YAKE 19

KAGERE AFUNGUKIA MATESO YA MABAO YAKE 19


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa haikuwa rahisi kufunga mabao 19 msimu huu wa 2019/20 kwenye Ligi Kuu Bara kutokana na mabeki wengi kumpania kumuumiza.
Simba ikiwa imefunga mabao 63 baada ya kucheza mechi 28 ikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake 71, Kagere ni kinara wa kucheka na nyavu akiwa na mabao 19 kibindoni.
Akizungumzia mabao yake 19 ya kwenye ligi, Kagere amesema:”Ni ngumu kufunga kutokana na mabeki wengi kuwa macho na mimi muda mwingi tukiwa uwanjani wanapambana, wanatumia nguvu nyingi kunikaba jambo ambalo limekuwa likinifanya nami ninakomaa na nikipata nafasi ninafunga,”.
Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuendelea Juni 13 kwa mchezo kati ya Yanga na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage ambapo Simba itashuka uwanjani Juni 14 ikimenyana na Ruvu Shooting.
SOMA NA HII  MWAMBA KAGOMA KUSEPA NANI ATOKE SIMBA !?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here