Home Uncategorized KIUNGO FUNDI WA SIMBA SASA KUIBUKIA YANGA, APIGWA MIAKA MIWILI

KIUNGO FUNDI WA SIMBA SASA KUIBUKIA YANGA, APIGWA MIAKA MIWILI


INAELEZWA kuwa kiungo wa zamani wa Klabu ya Simba aliyetwaa tuzo ya kiungo bora ndani ya Simba kwa msimu wa 2018/19 anaweza kuibuka muda wowte ndani ya Yanga kwa kuwa ni mchezaji huru.

Kotei alipomalizana na Simba aliibukia Klabu ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini mambo yalipokuwa magumu akaibukia Klabu ya FC Slavia-Mozŕy ambako huko taarifa zinaeleza kuwa amevunja mkataba hivyo kwa sasa ni mchezaji huru.


Habari zinaeleza kuwa tayari Kotei ameshamwaga saini ya miaka miwili ndani ya Yanga kinachosubiriwa ni wakati wa kutambulishwa ndani ya Yanga.

Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga amesema kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa wakati wa usajili haujafika.

SOMA NA HII  LIGI KUU SIO KITOTO TENA SIMBA,YANGA JUMAMOSI HII

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here