Home Uncategorized KMC KUKINUKISHA NA AZAM KESHO KAMA KAWAIDA, WAPEWA ONYO

KMC KUKINUKISHA NA AZAM KESHO KAMA KAWAIDA, WAPEWA ONYO


SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeruhusu mechi za kirafiki kuchezwa Ila kwa kibali kutoka TFF ili kuhakikisha wahusika wanafuata mwongozo wa Wizara ya Afya ya mwongozo wa kujikinga na Virusi vya Corona unazingatiwa.

Uamuzi huu umefikiwa leo kwenye kikao cha pamoja cha TFF na viongozi wa Vilabu vya Simba, Yanga, Azam FC, KMC na Transint Camp.

Vilabu hivyo pia vimeomba radhi kwa TFF na Serikali kwa kukiuka mwongozo kutoka Wizara ya Afya kwa mechi za kirafiki walizocheza bila kufuata tahadhari.


Mchezo wa kesho wa kirafiki kati ya Azam FC na KMC ndio utaanza utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa leo.


SOMA NA HII  YANGA: TUPO VIZURI KWA MSIMU UJAO