Home Uncategorized MATOLA – TUTATANGAZA UBINGWA MBEYA

MATOLA – TUTATANGAZA UBINGWA MBEYA

BAADA ya ushindi wa juzi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui, benchi la ufundi la Simba limesema harakati za kutangaza ubingwa kwao zinaanzia mkaoni Mbeya.

Simba juzi ilifikisha pointi 75 baada ya kuifunga Mwadui, ukiwa ni mchezo wao wa 30, hivyo kuhitaji pointi nane tu kutoka katika mechi zao nane zilizobaki kutangaza ubingwa.

Pointi hizo zitaiwezesha Simba kufikisha pointi 83 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote Ligi Kuu Tanzania Bara, si Azam itakayotimiza pointi 82 wala Yanga watakaokusanya pointi 80 iwapo watashinda michezo yao yote iliyobaki.

Akizungumza mara baada ya mchezo wao na Mwadui FC, Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola, alisema kuwa safari ya kutangaza ubingwa itaanzia Mbeya pale watakapocheza mechi mbili na kuvuna alama sita.

“Tunakwenda Mbeya kucheza mechi mbili ambazo tunahitaji ushindi ili kupata alama sita zitakazotufikisha pointi 81, huku tukiangalia matokeo ya kesho (jana) ya Azam watakapocheza na Yanga.

“Kama Azam watashinda mechi yao na Yanga, watatuongezea safari ambayo tutakuja kutangaza ubingwa Mtwara tutakapokwenda kucheza na Ndanda, lakini akipoteza tu, ubingwa tutatangaza tukiwa Mbeya tukicheza na Tanzania Prisons,” alitamba Matola.

Katika mchezo baona ya Azam na Yanga jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu hizo zilitoka suluhu.

Matola alisema wanakila sababu ya kutangaza ubingwa mapema lakini lazima wapambane na kumapata matokeo ya alama tatu ambazo zitatimiza wanachohitaji.

“Kama wachezaji watafanya makosa yoyote yatakayosababisha tupoteze mchezo, yatatuongezea safari na kuifanya iwe ngumu, hivyo lazima hili suala litimie mapema sana.”

Simba inatarajia kuanza safari ya kuelekea mkoani Mbeya leo kucheza na Mbeya City Jumatano kabla ya kuivaa Tanzania Prisons wikiendi hii.

SOMA NA HII  BEKI MKENYA AJIPELEKA MWENYEWE SIMBA ASAINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here