Home Uncategorized MBELGIJI WA YANGA KUTUA LEO

MBELGIJI WA YANGA KUTUA LEO


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael anatarajiwa kutua leo kwa ajili ya kuendelea kibarua chake majira ya saa 7:20 mchana.

Eymael alielekea Ubelgiji baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo kutokana na janga la Virusi vya Corona, Machi 17.

Sababu ya kuchelewa kurejea Bongo ni kufungwa kwa anga nchini Ubelgiji ambapo ilitokana na janga la Virusi vya Corona.

Wakati akiwa Ubelgiji, Yanga ilikuwa chini ya Kocha Msaidizi Charles Mkwassa na leo kikosi kimeanza safari kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi utakaochezwa Juni 14 Uwanja wa Kambarage. 

SOMA NA HII  KAGERE ANA BALAA KINOMA UWANJANI, MABAO YAKE NI ZAIDI YA 40