Home Uncategorized MIPANGO YA BIASHARA UNITED NI MOTO

MIPANGO YA BIASHARA UNITED NI MOTO


UONGOZI wa Biashara United umesema kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kushinda mechi zake zilizobaki ili kufaniksha malengo waliyojiwekea.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwenyekiti wa Biashara United, Seleman Mataso amesema kuwa wanapita kwenye kipindi kigumu kwa kutokuwa na fedha za kutosha hilo haliwapi tabu kufikia malengo ambayo wanayafikiria.

“Kuna ugumu kwa sasa kwenye ligi kutokana na ushindani uliopo kwa sasa, malengo yetu ni kuona tunamaliza nafasi tano za juu.

“Ili kufika malengo hayo ni lazima kushinda mechi ambazo zimebaki na inawezekana kwa kuwa wachezaji wapo tayari na morali ni kubwa,” amesema.

Mchezo wa Juni 20, Ndanda ilifungwa bao 1-0 mbele ya Ndanda FC, Uwanja wa Nangwanda.

SOMA NA HII  OSCAR MASAI, OBREY CHIRWA KUIKOSA JKT TANZANIA KESHO