Home Uncategorized MORRISON: NILICHEZA MECHI MBILI BILA KUWA NA MKATABA NDANI YA YANGA

MORRISON: NILICHEZA MECHI MBILI BILA KUWA NA MKATABA NDANI YA YANGA


BERNARD Morrison, nyota wa Klabu ya Yanga amesema kuwa alicheza mechi mbili akiwa hajasaini dili na klabu hiyo kwa kuwa walikuwa wakihitaji kutazama uwezo wake kwanza.

Morrison alitua ndani ya Yanga akiwa mchezaji huru akitokea nchini Ghana ambapo alisajiliwa kwenye usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari.

Morrison amesema kuwa kazi alikubali kucheza mechi hizo kwa kuwa ana mapenzi na Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Luc Eymael.

“Nilicheza mechi mbili awali baada ya kuja Bongo ambapo ilikuwa ile ya kwanza mbele ya Singida United ambapo tulishinda baada ya hapo nikamalizana nao kwa kusaini dili na Yanga.

“Kuna mengi ambayo ninafanya na yote ni kwa mapenzi na klabu ya Yanga kwa kuwa huku tunashirikiana vizuri na tunaishi tukiwa ni familia ndio maana nikipata nafasi ninatimiza wajibu wangu bila matatizo,” amesema.

Morrison ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda FC utakaochezwa Uwanja wa Taifa kwa kuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi mbili kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons.

Akiwa amecheza mechi 11, Morrison ametupia jumla ya mabao matatu na ana pasi tatu za mabao ndani ya Yanga kwenye Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  MTIBWAR SUGAR YAKOMAA NA MATATIZO YAO WENYEWE, KICHAPO MBELE YA MBEYA CITY CHAIBUA HAYA