Home Uncategorized MWADUI FC: TUPO TAYARI KWA LIGI

MWADUI FC: TUPO TAYARI KWA LIGI


UONGOZI wa Mwadui FC umesema kuwa utapambana kwenye mechi zake zilizobaki ili kupata matokeo chanya.

Akizungumza na Saleh Jembe, meneja wa Mwadui FC, David Chakala amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote zilizobaki kwa kuwa wachezaji wapo tayari.

“Kila kitu kipo sawa kwa sasa hasa ukizingatia tayari masuala ya michezo yameruhusiwa,wakati wachezaji wapo mapumziko walikuwa wanapewa program na Kocha Mkuu, Khalid Adam hivyo hakuna kilichoharibika.

“Tunachosubiri kwa sasa ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu tutakazocheza kwani tunajua ushindani utakuwa mkubwa,” amesema.

Juni 13, Mwadui FC itamenyana na Yanga, Uwanja wa Kambarage mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa kwanza.

SOMA NA HII  VIDEO: GUMZO SAUTI YA MORRISON KUHUSU MAMILIONI YA SIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here