Home Uncategorized OLE GUNNAR SOLSKJAER AMTAJA POGBA KUWA MCHEZAJI BORA DUNIANI

OLE GUNNAR SOLSKJAER AMTAJA POGBA KUWA MCHEZAJI BORA DUNIANI


OLE Gunnar Solskajaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa kiungo wake Paul Pogba ni miongoni mwa wachezaji bora ulimwenguni kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja.
Pogba, mwenye miaka 27 aliwashangaza wengi kwa kuonyesha uwezo mkubwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham kwa kutimiza majukumu yake vema na kuhusika kwenye pointi moja ambayo waliipata Manchester United wakati wakilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.
Akitokea benchi dakika ya 63 kwenye mchezo huo wakati United ikiwa imefungwa bao 1-0 na Tottenham iliyo chini ya Kocha Mkuu, Jose Mourinho, bao hilo lilifungwa na Steven Bergwijn dakika ya 27 ambapo United walifunga bao dakika ya 81 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Bruno Fernandes.
Penalti hiyo ilisababishwa na Pogba baada ya kuchezewa faulo ndani ya box na Eric Dier, sare hiyo inawafanya United wafikishe jumla ya pointi 46 wakiwa nafasi ya tano huku Tottenham ikifikisha pointi 42 nafasi ya nane na zote zimecheza mechi 30. 
“Kipindi cha pili kwa namna ambavyo tumecheza tulistahili kupata pointi tatu lakini hakuna tatizo tumeanza vizuri, wachezaji wangu wamecheza vizuri, Pogba amefanya makubwa na ni mchezaji bora ndani ya ulimwengu kwa sasa kwa kuwa ana vitu vingi,” amesema.
 Pogba hakuwa uwanjani kwa muda mrefu tangu Desemba mwaka jana ambapo alikuwa akisumbuliwa na majeraha.
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here