Home Uncategorized SIMBA KWA SASA HAIPO TAYARI KUONA WACHEZAJI WAKIANZA LIGI, SABABU HII HAPA

SIMBA KWA SASA HAIPO TAYARI KUONA WACHEZAJI WAKIANZA LIGI, SABABU HII HAPA


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa iwapo ataulizwa kwa sasa kama anaweza kuruhusu timu yake kurejea uwanjani hatakubali kwa kuwa wachezaji wake hawajawa na utimamu wa mwili.

Simba imeripoti kambini Mei 27 na kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na zile za Kombe la Shirikisho.

Ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 kibindoni imetupia mabao 63.
Kuhusu kurejea kwa ligi Sven amesema“ Ukiniambia kuwa kwa sasa tupo tayari kucheza nitakwambia hapana, sababu wachezaji hawana utimamu wa mwili.

” Kwa hizi wiki mbili zilizobaki kabla ya ligi kurejea zitatusaidia kutuweka vizuri.Tayari nimewaanzishia wachezaji program ya mazoezi ambayo itawarudisha taratibu kwenye ubora wao.”
Juni 13 ligi kuu Bara inaanza kutimua vumbi baada ya Serikali kuruhusu kuanza kwa masuala ya michezo iliyosimamishwa tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

SOMA NA HII  MCHAMBUZI AMPA USHAURI HUU ROBERTINHO LEO DHIDI YA AL AHLY