Home Uncategorized SIMBA WAAMBIWA WAACHE MANENOMANENO

SIMBA WAAMBIWA WAACHE MANENOMANENO

BAADA ya kupata sare ya kufungana bao 1-1, Uongozi wa Ruvu Shooting umesema kuwa Simba ina kazi ya kujipanga iwapo ina nia ya kupata ubingwa kwani wachezaji wake hawana pumzi.
Juni 13, Simba ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 ambapo, Shiza Kichuya alifunga kwa Simba na Fully Maganga aliweka mzani sawa kwa Ruvu Shooting.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa anashangaa kuona Simba inatamba ina kikosi kipana ilihali imepona  kufungwa mabao nane kutokana na wachezaji wake kukosa pumzi.
“Nashangaa kuskia kwamba wapinzani wetu wanatamba wanahitaji kutwaa ubingwa na mechi zao walitenga nne, ajabu kweli! Niliwaambia mwanzo waitoe Ruvu kwenye hiyo orodha kwani tumeona wachezaji wake hawana pumzi kabisa.
“Iwapo ingetokea tukaambiwa turudi tena uwanjani, sidhani kama wangeweza kupambana, wanapaswa wajipange upya ili kujiita wana kikosi kipana na wanahitaji ubingwa hakuna kitu, ni manenomaneno tu,” alisema Bwire.
SOMA NA HII  MAHAKAMA YAMPIGA 'STOP' MORRISON SIMBA