Home Uncategorized SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI MBEYA CITY LEOLEO

SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI MBEYA CITY LEOLEO


BAADA ya kikosi cha Simba kufika jijini Mbeya leo kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kuvaana na Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck itashuka Uwanja wa Sokoine, Juni 24 kumenyana na Mbeya City.

Mchezo huo utakuwa ni wa 31 kwa Simba sawa na Mbeya City iliyo chini ya Kocha Mkuu, Amri Said.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi zake 75 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 18 na kibindoni ina pointi 30, zote zimecheza mechi 30.

SOMA NA HII  COASTAL UNION: TUNA MBINU MPYA ZA KUIMALIZA SIMBA LEO