Home Uncategorized SINGIDA UNITED HALI BADO NI TETE

SINGIDA UNITED HALI BADO NI TETE

KUPOTEZA kwa kufungwa mabao 2-0 jana Juni 20 mbele ya JKT Tanzania kunazidi kuizamisha kwenye ugumu wa kujitoa kwenye mstari wa kushuka daraja Klabu ya Singida United.

Jana Uwanja wa Jamhuri, Singida United ilishindwa kufurukuta mbele ya JKT Tanzania na kukubali pointi tatu kuyeyuka jumla.

Mabao ya JKT Tanzania yalipachikwa kimiani na Musa Said dakika ya 11 na Hafidh Mussa dakika ya 61.

Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 30, imebakiwa na mechi nane ili kukamilisha mzunguko wa pili.

SOMA NA HII  SIMBA: YANGA WAISHUKURU GSM BILA WAO KUTUFUNGA INGEKUWA NDOTO