Home Uncategorized TIMO WERNER AKUBALI KUIBUKA CHELSEA

TIMO WERNER AKUBALI KUIBUKA CHELSEA

CHELSEA, inaonekana ina nafasi kubwa ya kuipoteza klabu ya Liverpool kupata saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig, Timo Werner.
Timo Werner, amekubali kujiunga na Klabu ya Chelsea licha ya kwamba amekuwa akihusishwa kujiunga na Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp kwa mujibu wa ripoti.

Liverpool imevutiwa na uwezo wa Werner raia wa Ujerumani mwenye mabao 31 kwenye mashindano yote msimu huu.

Lakini kwa sasa Chelsea imesema kuwa imefikia makubaliano mazuri na mchezaji huyo mwenye miaka 24 ambaye ameonyesha nia ya kutua ndani Stamford Bridge msimu ujao.

Dili atakalosaini inaelezwa ni la mkataba mrefu ambapo mkwanja pia utakuwa mnono kwa wiki jambo ambalo limemfanya nyota huyo asipinge suala la kuibukia ndani ya Chelsea.

Makubaliano ya Chelsea na Leipzig yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni huku Liverpool wakigomea kukutana na Werner  ili kufanya naye mazungumzo.
SOMA NA HII  HUKO AZAM FC HAKUNA UTANI TENA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here