Home Uncategorized UBINGWA SIMBA UNABEBWA KWA HESABU HIZI HAPA

UBINGWA SIMBA UNABEBWA KWA HESABU HIZI HAPA

SARE ya jana, Juni 21 kati ya Yanga dhidi ya Azam, Uwanja wa Taifa imezidi kuisogeza Simba katika kuufikia ubingwa.

Iko hivi, Simba wakishinda mechi mbili za Mbeya, ambazo ni dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons watabakiza sare tu kutwaa ubingwa na ili iwe hivi lazima Yanga na Azam nao wawe wameshinda mechi zao zote mbili.

Twende kimahesabu sasa

Azam FC- imekusanya pointi 58 baada ya kucheza mechi 30 imebakiwa na mechi nane ambazo ni sawa na pointi 24.


Hivyo ukichukua 58+24=82

Yanga SC imecheza mechi 30 kibindoni ina pointi 56 imebakiwa na mechi 8 ambazo zina pointi 24.


Hivyo ukichukua 56+24=80

Simba SC imecheza mechi 30 ina pointi imebakiwa na mechi 8 ambazo ni sawa na pointi 24.


Ikiwa itashinda mechi zake mbili na kupata sare moja itajiwekea kibindoni pointi saba ambazo zitaipa ubingwa kwa kuwa ina mabao mengi ya kufunga tofauti na Azam FC ambao wanaweza kufikisha pointi 82.

Itakuwa namna hii 75+7=82.

Ikiwa itashinda mechi zake zote nane itakuwa namna hii:-75+24=99

 Kama Yanga au Azam wote watapata sare au kupoteza mechi moja, Simba akishinda zote Mbeya, tayari atakuwa bingwa.

Kwa Azam na Yanga sasa zinachuana vikali katika nafasi ya pili. Kuchukuana kwao huko kuna ongeza nguvu ya kuichelewesha Simba kubeba ubingwa mapema zaidi.

SOMA NA HII  ALY KAMWE AWATUPIA KIJEMBE HIKI SIMBA PACOME AHUSISHWA