Home Uncategorized UONGOZI WA SIMBA WAIPIGIA HESABU NDEFU AZAM FC KESHO TAIFA

UONGOZI WA SIMBA WAIPIGIA HESABU NDEFU AZAM FC KESHO TAIFA


UONGOZI wa Simba umesema kuwa unautazama mchezo wa kesho wa hatua ya robo fainali kwa upekee licha ya wachezaji wake kutoka kupambana mechi mbili mfululizo nje ya Dar es Salam.

Simba ilicheza mechi mbili Mbeya ambapo ilianza kumenyana na Mbeya City Uwanja wa Sokoine na ilishinda mabao 2-0 kisha ikamalizana na Tanzania Prisons kwa kulazimisha sare ya bila kufungana.

Ikiwa tayari imeshatangazwa kuwa mabingwa, jana ilirejea kutoka Mbeya na leo imeanza maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Azam FC utakaochezwa kesho Uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa anatambua utakuwa mchezo mgumu ila wachezaji wake wapo tayari.

“Ni mchezo mgumu kwetu na utakuwa na ushindani mkubwa hilo lipo wazi lakini nasi tumejipanga kuona namna gani tutapata matokeo mazuri.

“Tumetoka kucheza mechi mbili hivi karibuni ambazo zilikuwa ni ngumu kwetu licha ya kwamba tumeshafanikisha lengo la kutwaa ubingwa bado tunahitaji kushinda mbele ya Azam FC,” amesema.

Mchezo huo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku.

Mshindi wa mchezo huo atamenyana na mshindi wa mchezo kati ya Yanga na Kagera Sugar utakaochezwa leo Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  SIMBA YAMPA MILIONI 173 MORRISON, PANGA LAPITA YANGA, NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU