Home Uncategorized WERNER AKUBALI KUSAINI CHELSEA, MANCHESTER UNITED NA LIVERPOOL KWA VIGEZO

WERNER AKUBALI KUSAINI CHELSEA, MANCHESTER UNITED NA LIVERPOOL KWA VIGEZO

TIMO Werner nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya RB Leipzig inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga amesema kuwa anaweza kusaini kwenye timu zote tatu ambazo zinahitaji saini yake kwa sasa iwapo mojawapo kati ya hizo itatimiza masharti yake.

Miongoni mwa timu ambazo zinampigia hesabu nyota huyo ni pamoja na Chelsea ambayo inapewa nafasi kubwa ya kupata saini ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 24.

Mbali na Chelsea pia Inter Milan, Manchester United na Liverpool nazo pia zimeonyesha nia ya kupata saini ya  nyota huyo  ambaye anapenda kwenda kucheza ndani ya Ligi Kuu England.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa fedha kwake sio jambo la msingi ila anachotazama ni malengo ya timu kufika mbali na kutwaa mataji.

” Fedha kwangu sio sababu ya mimi kwenda kucheza ama kusaini ingekuwa hivyo ningependa kucheza China, ila kwa kuwa Liverpool, Chelsea na United zinanitaka sawa ninaweza kusaini kwa timu ambayo itakuwa bora kwangu,” amesema.

SOMA NA HII  XAVI HERNANDEZ ATAKA KUINOA BARCELONA