Home Uncategorized YANGA: TUPO TAYARI KUIVAA MWADUI FC, WAMSHUKURU MUNGU KUWALINDA

YANGA: TUPO TAYARI KUIVAA MWADUI FC, WAMSHUKURU MUNGU KUWALINDA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa Juni 13 Uwanja wa Kambarage.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa ni jambo la kusmhukuru Mungu kwa kuwa wamefika kambini salama.

“Safari yetu ilikuwa nzuri na tulifika jana kwani hapa sio mbali ukizingatia kwamba tulikuwa na usafiri wetu wa basi, ila tulipata hitilafu kidogo ambayo ilikuwa ni ajali hilo halipo juu ya uwezo wetu, hakuna anayeomba ajali.

“Licha ya ajali hiyo bado Mungu alitupigania na tumetoka salama katika hilo kwani tairi lilipata hitilafu kisha tukaendelea na safari, kwa sasa tunaanza maandalizi ya kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mwadui tuna amini tutafanya vizuri,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 27 za ligi. 

SOMA NA HII  HAWA HAPA MASTAA WATANO WENYE MKWANJA MREFU AFRIKA